MAHITAJI/INGREDIENTS.
1.Chocolate Nyeusi vipande 20
20 bars Dark Chocolate
2.Chocolate Nyeupe vipande 18
18 bars white Chocolate
3.Peanut butter kijiko cha chakula 1
1 Tbsp Peanut butter
4.Blue band kijiko cha chai 1
1 Tea spoon Butter
MAANDALIZI/PREPARATIONS.
1.Chukua tray ya pembe nne weka foil likandamize lifate umbo la ndani ya tray huku foil jengine libakie juu uweze kuishika wakati wa kuitoa
Line rectangular pan with aluminum foil, leaving 1 inch of foil overhanging at 2 opposite sides of pan
2.Chukua siagi(Blue Band)pakaa kwenye foil lako hakikisha inaenea kote ndani ya tray
Butter the pan make sure you spread all over the foil.
3.Vunja vunja chocolate nyeusi vipande vidogo vidogo na weka kwenye bakuli
Break the dark chocolate into small pieces and keep them in the bowl
4.Weka Peanut butter kwenye kibakuli chenye chocolate nyeusi
Add peanut butter in the bowl that contain dark chocolate
JINSI YA KUTAARISHA/HOW TO PREPARE
1.Yeyusha kwenye microwave kama huna naelezea jinsi ya kuyeyusha kwa njia ya kawaida hatua ifuatayo
Melt the mixture in the microwe till melted otherwise use the next step
2.Chukua sufuria weka maji kidogo kisha juu yake weka bakuli la bati
Take a pan and add small amount of water and keep metal bowl on top of it
3.Washa jiko moto wa kiasi acha maji yachemke
Turn the flame let the water boil
4.Weka mchanganyiko wako kwenye bakuli la bati huku ukikoroga mpaka uwe rojo
Add the mixture in the bowl and steer well till melted
5.Ukiyayuka mimina kwenye tray ueneze kote
When completely melted pour on the tray and spread it
6.Yeyusha chocolate nyeupe katika chombo kengine na umimine kwenye mchanganyiko wa mwanzo
Melt the white chocolate in separate bowl then pour on top of the previous mixture in the tray
7.Chukua kijiko kigeuze,shika kule kwa kulia kisha changanya mchanganyiko wako kupata huo muonekano wa Zebra
Use spoon handle mix the mixture randomly to get Zebra view
8.Weka kwenye friji kwa masaa 12(Nusu siku) au siku nzima
Refrigerate for 12 Hours or the whole day
9.Itoe kwenye friji kata kata vipande kwa umbo upendalo
Remove from the frige,use a knife to cut into any shape you prefer
10.Unaweza kula na kahawa au zenyewe
You can serve with coffee or as it is
Angalizo:Note
1.Usizidishe kiwango cha peanut butter utaibadilisha rangi,ladha na itakuwa nzito
Do not add too much peanut butter cause to change the taste,colour and consistency
2.Ukiyayusha chocolate kwa njia ya kawaida hakikisha haingii maji
Make sure the chocolate do not contaminate with water when melted on the stove
3.Ukisha kuikata iliwe yote au iliwe na kuhifadhiwa kwenye friji la sivyo inayayuka
After you cut them into pieces eat them or if you are not ready take them back to the fridge otherwise will melt
Furahia Fagi Zako.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni