Pages

Pages - Menu

Jumatatu, 25 Aprili 2016

COOKING GREEN BANANA WITH CHICKEN (NDIZI KUKU ZA TUI LA NAZI)


MAHITAJI/INGREDIENTS
1.Ndizi mbichi 12(Malindi)
 12 Green Banana

2.Kuku Nusu
 Half of Chicken in pieces

3.Nyanya kubwa(Tungule) 4
 4 Medium sized Tomatoes

4.Nazi moja kubwa
 1 Coconut (OR)coconut powder

5.Ndimu 1
 1 Lemon

6.Karoti 1
 1 Carrot

7.Pilipili Hoho(Pilipili boga)1
 1 Green Pepper

8.Kitunguu maji kikubwa 1
 1 Onion

9.Nyanya ya Paket vijiko vya chakula 2
 2 Tbsp of Tomato Paste

10.Royco(Sio lazima)
 Royco OR Any Masala(Optional)

11.Tangawizi na kitunguu thomu ilotwangwa kijiko cha chakula 1 
 Mixture of Garlic with Ginger

12.Vitunguu thomu punje 3 kwa ajili ya Mchuzi
  3 Garlic Cloves for blended tomato

13.Chumvi Kiasi
  Salt to taste

MAANDALIZI/PREPARATION
1.Osha viungo vyako vyote vinavyotakiwa kuoshwa
 Wash all ingredient if needed

2.Katakata Nyanya,Kitunguu maji,thomu,Pilipili hoho weka kwenye blenda na uvisage vyote
  Cut tomato,onion,green pepper,garlic and add them into jug then blend them

3.Loweka ndizi mbichi kwenye maji ili upunguze utomvu
  Soak the banana into big bowl 

4.Menya Ndizi zipare na kata kata kwa umbo unalolipenda
  Peel them and grate a little bit to remove upper layer of it then cut them to any size you prefer

5.Kuna nazi yako na ichuje
  Prepare the fresh coconut to get the coconut milk if you use Fresh Coconut instead of Coconut Powder

4.Weka tui zito na jepesi mbalimbali
 Separate heavy Coconut milk And light one during preparation

JINSI YA KUPIKA/HOW TO COOK
1.Chemsha kuku ulomuweka tangawizi kitunguu thomu na chumvi mpaka awive muache na supu kiasi
 Boil the chicken added mixture of garlic and ginger,with salt till cooked

2.Chukua sufuria nyengine chemsha ndizi na chumvi kiasi mpaka ziive kisha mwaga maji weka pembeni
   Use a separate Cooking Pot to Boil the banana added salt till cooked, then pour the remain water and leave the banana dry in the pot

3.Weka nyanya ulizozisaga kwenye nyama yako acha ziive
  Add the mixture of Tomato in your cooked chicken

5.Weka nyanya ya paketi na Royco
  Add tomato paste And Royco

6.Weka chumvi na ndimu acha kwa dakika 1 na uonje mchuzi wako kama hauja chapuka ongeza chumvi kidogo
 Add salt and lemon juice and taste it after 1 minutes,if its okay remove from the heat if  not Ok,add little salt in it

7.Weka tui jepesi kwenye ndizi na chumvi acha zichemke kwa dakika 5 usikoroge
 Add light coconut milk with salt in the pot that having banana and let them cooked for at least 5 minutes don't use spatula to mix it 

8.Kisha weka tui zito acha lichemke kwa dakika 3
 Then add the heavy coconut milk and leave it for 3 minutes

9.Weka mchuzi wako wa nyama acha kwa dakika 2 epua
 Add the mixture of Chicken with tomato you cooked before and leave it for 3 minutes

10.Acha zipoe kidogo pakua kwenye sahani tayari kwa kula
 Let them cool ready to serve

NB1.Hakikisha mchuzi unakua mzito mzito na mdogo
           Make sure the cooked mixture of chicken with tomato is too heavy 

       2. Pika ndizi zako kwa moto wa wastani ili zisigande kwenye sufuria
           Prepare your dish into medium heat

       3.Epuka kukoroga wakati wa kuzipika ndizi zako
         Don't mix it by using spatula during cooking this dish

       4.Kama utataka kukoroga chukua tambara safi shika sufuria yako itikise au chukua banio la ugali bana kwenye sufuria na uitikise
     If you want to mix use a clean towel and take your cooking pot and shake it a little bit

      5.Unaweza kupika kwa Samaki,Nyama,Dagaa pia ukipenda
       You can use Fish,Meat instead of Chicken

Furahia Ndizi Zako.

Maoni 1 :

  1. Safi sana, Hongera kwa Maelezo Mazuri. Be Bleesed 🙏

    JibuFuta