Pages

Pages - Menu

Jumatano, 2 Desemba 2015

WALI WA KUKAANGA(VEGETABLE FRIED RICE)


MAHITAJI
1.Mchele wa basmat nusu kilo
2.Karoti kubwa 1
3.Pilipili boga(Pilipili hoho) kubwa 1
4.Kitunguu maji kikubwa 1
5.Mafuta kiasi
6.Chumvi kiasi
7.Maji kiasi

MAANDALIZI
1.Osha mchele wako kisha uweke maji kiasi
2.Loweka mchele kwa nusu saa
3.Para karoti yako weka pembeni
4.Kata kata vitunguu maji na pilipili hoho weka pembeni

JINSI YA KUPIKA
1.Weka kikaangio jikoni kisha tia mafuta
2.Anza kukaanga vitunguu maji kisha pilipili boga na malizia karoti
3.Usivikaange sana mpaka vikawa brown kama vya mchuzi
4.Toa viungo vyako weka kwenye kibakuli na mafuta yake
5.Chukua sufuria ya kupikia wali mimina maji ulio rowekea mchele
6.Yaweke chumvi na weka jikoni yapate moto
7.Acha yachemke kisha weka mchele na uache uive
8.Acha maji yakauke kidogo mimina vitu ulivyo vikaanga na mafuta yake kwenye wali wako
9.Acha ukauke na uive vizuri
10.Pambia ila hakikisha haufanyi matandu
11.Pakua tayari kwa kula na kitu chochote upendacho
NB: 1.Hakikisha viungo havikaangwi sana
       2.Usiache wali ukauke kabisa kabisa ndio uviweke viungo
       3.Usiongeze mafuta zaidi uliyo kaangia kwenye wali

Furahia Wali Wako

Maoni 1 :

  1. mchele kilo 1 unapikwa na maji kiasi gani naomba nijibu kwa email gilegodly@gmail.com

    JibuFuta