MAHITAJI/INGREDIENTS
1.Unga wa Ngano Vikombe
4
4 Cups Plain
Purpose Flour
2.Maziwa ya maji Kikombe
1
1 Cup Milk
3.Mayai 2
2 Eggs
4.Hamira Vijiko vya
Chakula 2
2 Tbsp Yeast
5.Siagi Vijiko 2
2 Tbsp Butter
6.Sukari Nusu Kikombe
½ Cup Sugar
7.Chumvi Kiduchu
Pinch of Salt
7.Chocolate ya Nutella Kikombe 1
1 Cup Nutella Chocolate
MAANDALIZI/PREPARATIONS
1.Changanya
maziwa(hakikisha yawe ya uvugu uvugu),hamira,unga kijiko kimoja na sukari
kijiko 1 koroga na acha mchanganyiko huo kwa dakika 10 ufure
Mix warm milk,yeast,one
table spoon of sugar and flour and dissolve all ingredients.Let it sit for 10
minutes to activate.
2.Chunga unga kwenye
bakuli na kisha toa nusu kikombe cha unga weka pembeni kwa ajili ya kusukumia
utakao bakia changanya na vitu vyote vikavu vilobakia yaani unga,sukari na
chumvi
In a large
bowl,sift the flour through a sieve. And remove half cup of the flour and keep
aside so as to use it for sprinkling .Then combine the dry ingredients
remained; flour,sugar and salt.
3.Vunja mayai toa viini
weka pembeni
Separate egg
yolks from egg whites.
4.Kisha weka viini,siagi
na hamira ilioumuka kwenye bakuli lenye mchanganyiko wa unga.
Add butter,egg
yolks and yeast in the bowl with dry ingredients
5.Chukua mwiko changanya
unga wako vizuri
Mix everything
with a wooden spoon.
6.Kanda unga wako kiasi
cha dakika 7
Knead the dough
for about 7 minutes
7.Ukipata donge laini
weka kwenye bakuli funika kwa kitambaa kisafi au plastic wrap katika sehemu ya
joto na acha kiasi cha nusu saa au mpaka liumuke vizuri.
Once you get
smooth dough,put it into a bowl and cover with plastic wrap or cloth and let it
rise for around 30 minutes or till double in size.
8.Nyunyiza unga sehemu
ya kusukumia donge na weka donge lako hapo
Place the
dough on a lightly floured surface.
9.Likande donge lako
kiasi cha dakika moja kasha ligawe sehemu 4
Knead the
dough for around 1 minutes and divide into 4 equal parts.
10.Chukua donge
moja sukuma katika umbo la chapati ila iwe na upana utakaozidi sahani
Roll the
first of four parts into circle the dough should be wider more then the size of
plate.
11.Kisha chukua karatasi
ya kuokea na weka lichapati lako juu ya ile karatasi.
Place the
dough circle on a piece of baking paper
12.Chukua sahani weka juu
ya chapati yako kisha kata sehemu zilozidi ibakie chapati yenye usawa wa sahani
Take a plate and
keep it on top of the circle and mark it to get the circle having same shape as
your plate.Cut the excess dough with a knife
13.Chukua Nutella kisha
pakaa kwenye duara lako vizuri hakikisha inaenea kote
Cover the
marked area with thin layer of chocolate spread.
14.Sukuma donge
jengine,na uliweke juu ya lile lenye nutella kisha ondoa sehemu zilozidi ili
liwe sawa na lile la mwanzo na pakaa nutella kama ulivyopaka la mwanzo
Roll
another layer of dough,place iton the previous one and mark off the plate on
it.Then put the chocolate spread on the marked area.
15.Sukuma donge la tatu
na rudia hatua zile zile tulizofanya kwa chapati ya kwanza na ya pili
Repeat the
procedure with the third dough.
16.Sukuma donge
lilobakia weka juu ya chapati tatu za mwanzo na weka sahani upate ukubwa sawa
na zile za mwanzo
Roll the last
dough into circle and put it on the previous layers and cover it with a
plate.Cut the excess dough with a knife
17.Chukua glasi ndogo
weka kati kati ya chapati yako ya juu
Using a
small keep it at the center of those circle.
18.Pasua chapati zako
sehemu nne sawa kisha pasua tena upate vipande nane endelea kupasua hadi
upate vipande 16 kumbuka unapasua bila kuitoa glasi yako pale kati
Divide the layers
into quaters ,start cutting from the marked circle without removing the glass
at the center.Divide the quarter into eight .At the end you should have 16
equal parts.
19.Kamata vipande viwili
kati ya 16 tumia mikono yote miwili na vizungushe mara mbili katika muelekeo
tofauti ,kimoja kizungushe kielekee kulia kingine kielekee kushoto.
Take two parts of
the 16 in both hands and delicately twist them in opposite directions.
20.Rudia kuzungusha kwa
vipande 14 vilivyobakia mpaka upate umbo kama kwenye picha hio chini
Repeat with
all pairs to form eight armed star
21.Ufunike sehemu ya
joto acha uumuke kiasi cha dakika 10
Cover it and let
it rise around for 10 minutes
22.Chukua ute wa yai
upige pige kisha pakaa juu ya mkate wako
Brush the surface
of the bread with egg white
JINSI YA KUPIKA/HOW TO COOK
1.Oka mkate wako kwa moto wa 180’C, kiasi cha dakika 15 mpaka 20
Bake at 180’C for around 15 to 20 minutes
2.Ukiona unapiga rangi ya dhahabu utoe kwenye jiko
When turn to golden colour remove from the oven
3.Acha upoe tayari kula na kinywaji upendacho.
Let it cool serve with any drinks you prefer
Furahia Mkate Wako Wa Nutella.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni