Pages

Pages - Menu

Alhamisi, 10 Desemba 2015

NDIZI NA SAMAKI(BOILED GREEN BANANA AND FRIED FISHES)


MAHITAJI
1.Ndizi Malindi 8
 8 Fresh Green Banana

2.Samaki(Tasi) 2
 2 Fishes

3.Pilipili ya kuwasha 
 2 Red chillis pepper

4.Kitunguu Thomu punje 4
 4 Garlic clove

5.Chumvi vijiko 
 2 Tbsp of salt

6.Maji 1500ml(Lita 1 na 1/2)
 Water 1 and 1/2 litre

7.Ndimu 1
 1 Lemon

8.Pilipili manga
 Black pepper powder

9.Soy sauce kijiko 1
 1 Tbsp Soy sauce

10.Mafuta robo lita
 1/4 litre of Sun flower oil

MAANDALIZI
-Ndizi:Banana
1.Chukua Bakuli kubwa weka ndizi zako kisha mimina maji lita 1
Take bananas in a bowl and pour 1 litre of water in it

2.Baada ya dakika 5 jiandae kumenya ndizi zako

After 5 minutes take a knife and get prepared to pel them

3.Chukua kisu kata ncha mbili za ndizi zako 

 Take a knife and cut the ends of the bananas off

4.Pasua ndizi yako kwa kuiweka alama 
Cut along each of the ridges

5.Menya ndizi na ziweke kwenye bakuli la maji safi 
Peel the skin away in sections and put the peeled banana in bowl of water

6.Zipare ndizi zako kisha zikata sehemu mbili sawa sawa
Grate the banana just slightly to remove a little upper layer and cut two equal pieces of each banana
-Samaki:Fishes
1.Osha vizuri samaki kwa kuondoa matumbo yote 
Wash them well and make sure you remove all dirt substance in them

2.Wakate kila mmoja vipande viwili kupata vipande vinne

Cut two pieces of each to get 4 pieces of fishes in total

3.Muunge vizuri kwa pilipili,pilipili manga,kitunguu thomu,chumvi kijiko kimoja na ndimu

Marinate them well with pepper,black pepper,garlic,lemon juice and 1 tbsp of salt

3.Kisha waache kwa robo saa

Leave them to be marinated well atleast quarter an hour

JINSI YA KUPIKA
-Ndizi:Banana
1.Chukua sufuria weka ndizi kisha mimina maji ya nusu lita yaliobakia
Put cutted banana in a pot and pour half litre of water

2.Weka chumvi kijiko kimoja

Put 1 tbsp of salt

3.Weka jikoni funika na ziache zichemke hadi ziive kuwa laini
Cover the pot and let it boiled in high medium heat till soft

4.Mwaga maji kama yamebakia 

Remove the pot and pour out the remained water

5.Weka ndizi zako kwenye sahani

Serve your banana in a plate
-Samaki:Fishes
1.Weka mafuta jikoni yaache yapate moto
Keep a pan on medium heat and let the oil be heated

2.Weka samaki akiwa brown mgeuze

Keep the fishes pieces and let it become brown

3.Mwache upande ulewa pili uive akiwa brown mtoe

Turn the other side let it becomes brown

4.Mchuje mafuta kisha muweke kwenye sahani

When its ready put the fishes on tissue paper so as to get dried from cooked oil

5.Nishaelezea vizuri jinsi ya kukaanga samaki unaweza rudia post yangu ya jinsi ya kukaanga samaki

For more details on how to fry fishes look my previous

Angalizo:Note
1.Hakikisha unapika ndizi hadi zinalainika
Make sure you boil the bananas till becomes soft

2.Kuwa makini usizichemshe mpaka zika vurugika

Dont over boil the banana

Furahia Ndizi Zako.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni