Is a Tanzanian Blog which prepare different food recipes found all over the world.Here you get the chance of reading Swahili and Non Swahili recipes found across the world.The recipes are written by two languages i.e Swahili and English.Welcome all to read and leave your comment about our recipes. Karibuni Nyote mjifunze mapishi ya Kiswahili na mengineo yanayopatikana dunia nzima.Karibuni mjifunze na tunakaribisha maswali na maoni tutakujibu haraka iwezekanavyo. Ahsanteni Sana.
Pages
▼
Pages - Menu
▼
Alhamisi, 10 Desemba 2015
KUKU LAINII WA KUKAANGA(FRIED SOFT CHICKEN)
MAHITAJI
1.Kuku nusu(Vidali 2)
2.Chumvi kijiko 1
3.Pilipili ya unga kijiko 1
4.Pilipili Manga nusu kijiko
5.Blue band kijiko 1
6.Mtindi robo kikombe
7.Mafuta nusu lita
8.Chicken Masala kijiko 1
9.Tangawizi ya unga kijiko 1
MAANDALI
1.Muoshe kuku vizuri na muweke kwenye bakuli safi
2.Weka blue band kwenye frying pan iache iyayuke
3.Muweke pilipili,chumvi,pilipili manga,blue band,mtindi,masala na tangawizi kisha mchanganye vizuri
4.Muweke kwenye friji akolee viungo kwa lisaa
JINSI YA KUPIKA
1.Weka mafuta kwenye karai na uyaweke jikoni
2.Acha yapate moto kiasi kisha weka kuku wako
3.Mwache aive mpaka afanye rangi ya brown
4.Kisha mgeuze upande mwengine
5.Endelea kumpika mpaka nyama yote iwe brown
6.Epua muweke kwenye tissue au chujio
7.Akipoa huyu kuku huwa mlainii na mtamu unaweza kula na chipsi,wali,mkate au chochote upendacho
Angalizo:
1.Usimpike sana hadi kukauka
2.Usiweke kuku kama mafuta hayajapata moto vizuri
Furahia Kuku Wako.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni