Pages

Pages - Menu

Alhamisi, 14 Julai 2016

EGG CHOP(MINCED MEAT EGG CHOP)


MAHITAJI/INGREDIENTS
1.Nyama ya kusaga kilo kasorobo(3/4)
 3/4 Kg Minced Meat

2.Kitunguu maji kikubwa 1
 1 Medium size Onion

3.Kerot kubwa 1
 1 Carrot

4.Pilipili Boga(Pilipili Hoho) kubwa 1
 1 Green Pepper 

5.Pilipili ya kuwasha ilotwangwa kijiko cha chai 1
 1 Tea Spoon Chopped Chilli

6.Kitunguu Thomu kilichotwangwa kijiko cha chakula 1
 1 Tbsp Crushed Cloves of Garlic

7.Tangawizi ilotwangwa kijiko cha chai 1
 1 Tea Spoon Minced Ginger

8.Pilipili Manga kijiko cha chai 1
 1 Tea Spoon Black Powder

9.Mayai 10
 10 Eggs

10.Mikate ya slesi 2
 2 Slice of Bread

11.Mafuta ya kupikia  Lita 1
 1 Litre Cooking Oil

12.Chumvi kiasi
 Salt to taste

13.Ndimu ilokamuliwa 1
 Lemon juice

14.Royco Vijiko vya Chakula 2
 2 Tbsp Royco

15.Uzile(Binzari Nyembamba ya Unga) Kijiko cha Chakula 1
 1 Tbsp Cumin powder

16.Maji kiasi
 Water 

MAANDALIZI/PREPARATION
1.Para keroti weka pembeni
 Grate carrots 

2.Para au kata pilipili boga weka pembeni
 Grate or chop the green paper

3.Pasua kati kitunguu maji kisha kikatekate kiweke pembeni
 Slice into halves the onion then chop it 

4.Vunja mayai mawili weka chumvi kiduchu kwenye bakuli kisha yapige kwa uma au kijiko
  Just crack two eggs in a bowl add little salt and bit them by a fork or spoon

5.Weka nyama robo kwenye sufuria ongeza na chumvi,ndimu,tangawizi na kitunguu thomu
 Put 1/4 of minced meat and add salt,lemon juice,ginger and garlic

6.Weka mayai 7 kwenye sufuria nyengine na chumvi kiasi
 Take another pan and add 7 eggs with water and salt

JINSI YA KUPIKA/HOW TO COOK
1.Weka nyama jikoni acha ichemke mpaka ikauke maji
 Boil the minced meat till dry

2.Weka royco kwenye nyama ichanganye kidogo kisha iepue
 Add royco and mix it for just 5 seconds

3.Chemsha mayai mpaka yaive
 Bring to boil the eggs in a pan

5.Ikaushe mikate ya slesi kwenye oven mpaka ikauke
 Take a slice into the oven bake them till dried

6.Ponda mikate kupata chenga chenga za Mikate kisha usiponde sana zikawa unga
  Crush the slice to get bread crumbs make sure the crumbs are not powdery

7.Changanya nyama mbichi na ile iloiva pamoja
 Mix the fresh minced meat remained and the cooked one together 

8.Weka Pilipili ya kuwasha kwenye nyama na uichanganye
 Add the chopped chilli and keep mixing

9.Weka pilipili manga,uzile na uendelee kuchanganya nyama yako
 Add the remaining spice as black pepper,cumin powder

10.Malizia kuweka Vitunguu maji,kerot na pilipili boga
 Finally add chopped onion,carrots and green pepper

11.Vunja yai lililobakia weka kwenye mchanganyiko wa nyama na kisha ichanganye vizuri
 Crack the final egg and add into the mixture after beating

12.Menya mayai yaliochemshwa
 Peel the Boiled eggs

13.Chukua nyama zungushia kwenye yai moja badala ya moja mpaka umalize mayai yote saba
 Take one egg and cover it with minced meat until you finish those 7 eggs

14.Nyunyizia chenga za mikate kwenye egg chop zako
  Sprinkle the bread crumbs on top of egg chops

15.Weka mafuta jikoni acha yapate moto mpaka yatoe moshi
 Heat the Oil to the maximum 

16.Chukua Egg chop ichovye kwenye mayai mabichi kisha weka kwenye mafuta
 Dip each Egg chop into the beaten eggs then fry them

17.Acha kwa dakika 2 au zaidi mpaka ijishike ndio unaweza kuigeuza
 Wait for 2 or 3 minutes before you flip it

18.Ukiona ina badilika  na kuwa ya rangi ya choklet itoe ichuje mafuta kwenye chujio au tissue
 When it turns to chocolate colour remove it from the pan and let it dry by using tissue or sieve

19.Malizia kuchoma zote mpaka zimalize
  Repeat the step till you finish the remaining 

20.Wacha zipoe kabisa ndio uzikate ama kula
 Let them cool completely before serve it

21.Unaweza kula zenyewe au na chatne ukipenda au mkate
 You can serve alone or with chatne,chilli,tomato paste or bread

Angalizo:Note
1.Kama una bread crumbs unaweza kutumia kama mbadala wa slesi za mikate
 You can use bread crumbs as a substitute of slice of bread

2.Usiweke unga wa ngano kabla ya kuzichoma kama mbadala wa bread crumbs 
  Don't use flour as a bread crumbs substitute

3.Hakikisha egg chop inazama kwenye mafuta wakati wa kuipika la sivyo itapasuka
 Make sure the Egg chop is deep completely in the oil otherwise it may break 

4.Ukiwahisha kuzigeuza wakati wa kuzipika zitapasuka
 Do not hurry to flip them otherwise it may break during frying

5.Ukiweka kabla mafuta hayajapata moto vizuri pia zitapasuka
   Do not fry them if the oil is not heated well

6.Unaweza kuongeza pilipili au viungo vyengine Zaidi upendavyo
 You can add more chilli or any spices you prefer

7.Ukiweka chumvi nyingi kwenye yai la nje husababisha egg chop kuwa na chumvi sana
 Do not add too much salt into the beaten egg otherwise the Egg chop will be too salty

8.Usiweke Egg chop nyingi wakati wa kupika ili usipate shida ya kuzigeuza na kutozipasua
 Do not fry many Egg chop at a time make sure there is a space in a pan between them so as you can easily flip them


Furahia Egg Chop Zako

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni