Pages

Pages - Menu

Jumanne, 31 Mei 2016

KUKU WA TANDOORI(TANDOORI CHICKEN)


MAHITAJI/INGREDIENTS
1.Kuku Mzima
 A whole Chicken

2.Tandoori(Rangi Nyekundu ya Unga) Robo Kijiko Cha  Chai 1
   1/4 Tea spoon Tandoori Powder

3.Chumvi Kiasi
  Salt to taste

4.Vinegar  Vijiko  Vya  Chakula  2
  2 Tbsp Vinegar  

5.Pilipilili ya kutwangwa  Kijiko  Cha  Chakula 1
  1 Tbsp Minced Red Pepper

6.Pilipili Manga kijiko Cha Chai 1
  1 Tea spoon Black Pepper

7.Mtindi  Robo Kikombe  Cha Chai
  1/4 Cup Plain Yogurt

8.Mafuta  ya Alizeti Vijiko Vya  Chakula 3
  3 Tbsp Sun Flower Oil

9.Tangawizi ilotwangwa Kijiko Cha Chakula 1
  1 Tbsp Grated Ginger

10.Kitunguu Thomu kilotwangwa Kijiko Cha Chai 1
 1 Tea spoon minced Garlic

11.Chicken Masala Kijiko Cha Chakula 1
 1 Tbsp Chicken Masala

12.Uzile(Binzari Nyembamba) kijiko Cha Chai 1
 1 Tea spoon Cumin seeds

MAANDALIZI/PREPARATION
1.Mkate Kuku  vipande  viwili sawa
  Slip the chicken into two halves

2.Muoshe vizuri kwa maji safi
 Rinse the halves well with clean water

3.Muweke Viungo vilotajwa hapo juu kasoro mafuta
 Marinate them well by adding the ingredients except oil

4.Vaa gloves za plastik waeneze vizuri viungo hadi wakolee
  Use plastic gloves to marinate them well

5.Weka kwenye friji kiasi cha masaa mawili au Zaidi
  Put them in the fridge atleast two hours or more

6.Ukiwatoa wamiminie mafuta waeneze vizuri na weka tayari kwa ajili ya kuwapika
  Remove from the fridge and pour the oil onto them 

JINSI YA KUPIKA/HOW TO COOK
1.Washa Oven Moto Nyuzi 180,weka moto wa juu na chini 
  Heat the oven by 180'C set the upper and lower heat

2.Weka kuku wako na wapike kwa saa moja(Dakika 60)
  Bake the Chicken for atleast an hour(60 minutes)

3.Kama jiko halina moto mkali usifungue jiko mpaka lisaa limalize
  If your oven heat is controllable don't open it,till the chicken are done

4.Baada ya lisaa kama hawajaiva vizuri pika tena kwa dakika 10 tu
  If you see they are not cooked well for an hour cook them for 10 minutes more

5.Baada ya huo muda wapo tayari kula na Chipsi au Wali
  After that time they are ready to serve them with chips,rice

Angalizo:
1.Kama jiko lina moto mkali pika kulingana na moto wa wastani wa jiko lako
 If your Oven is uncontrollable set the degree according to your Oven

2.Unaweza kumuweka kwenye friji  zaidi ya masaa 6 au siku nzima
  You can refrigerate them for 6 hours or a day 

3.Ikiwa jiko lako lina uwezo wa kuseti muda ni vizuri uweke muda wa lisaa kuepuka kufungua jiko mara kwa mara kwani husababisha joto kupotea
 If your Oven has timer better to set so as to avoid to loose heat when opening the ovening door

4.Unaweza kuweka Tandoori Zaidi kama utapenda kuku wako awe mwekundu Zaidi.
  You can add more Tandoori powder if you prefer dark red chicken

5.Unaweza Kumpika kwenye jiko la mishkaki kama hauna oven.
  You can bake in Grill or Barbeque stove if you dont have an Oven


Furahia Kuku Wako.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni