MAHITAJI
- Mbatata 8
- Nyanya(Tungule) ndogo 2
- Chumvi kijiko kidogo 1
- Mafuta vijiko vya chakula 4
- Tomato paste kijiko cha chakula 1
- Yai 1
- Kitunguu maji kidogo 1
- Royco kijiko 1
- Karoti ndogo 1
- Pilipili boga(Pilipili hoho) ndogo 1
MAANDALIZI
- Osha viungo vyako vyote weka kenye bakuli safi
- Menya viazi mbatata na kata kata vipande 4 kwa kila mbatata moja
- Kata kata kitunguu maji,keroti na hoho weka pembeni
- Para nyanya weka pembeni
- Vunja yai weka kwenye kibakuli lipige pige kama unataka kukaanga
JINSI YA KUPIKA
- Weka karai la mafuta jikoni acha yapate moto
- Weka viazi vyako vikaange mpaka vikaribie kuiva
- Weka viazi pembeni kisha kaanga vitunguu mle mle bila kutoa viazi
- Kisha weka pilipili hoho endelea kukaanga
- Malizia na karoti kaanga zikiwa za brown weka nyanya
- Koroga na uweke chumvi na royco kisha funika acha vichemke kwa dakika 1
- Weka nyanya ya paketi koroga funika kidogo kwa dakika 1
- Mimina yai koroga usiache mkono mpaka livurugike lote lifanye chenga nyeupe
- Epua acha ipoe tayari kula na Chapati,mikate yoyote,wali au ugali.
Angalizo:
- Usikaange viazi mpaka vikakauka na kuungua
- Usiache yai likagandana na viazi
- Usiweke maji kwenye upishi huu
- Hakikisha unafunika vizuri ukisha kuweka nyanya
- Usikaange kwa muda mrefu vitaganda kwenye karai
- Unaweza kuweka viungo vya pilau ukipenda pia
- Hakikisha tomato paste haiwi nyingi husababisha viazi kuwa vikali
Furahia Viazi Vyako.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni