Pages

Pages - Menu

Jumatano, 10 Februari 2016

VISHETI VYA MAZIWA(VIKOKOTO)


MAHITAJI/INGREDIENTS

1.Unga wa Ngano nusu kilo
 1/2 kg Flour

2.Sukari kikombe kimoja cha Rice Cooker
 1 Cup Sugar (Rice Cooker Cup)

3.Maji robo ya kikombe
 1/4 Cup of Water (Rice Cooker Cup)

4.Arki Vanilla kifuniko chake 1
 1 Cap Vannila Essence (Bottle Cap of Vannila)

5. Arki Ice Cream kifuniko chake 1
  1 Cap Ice Cream Essence (Bottle Cap of Ice  Cream)

6.Siagi(Blue Band) vijiko vikubwa  2
 2 Tbsp Butter

7.Custard kijiko kikubwa 1 
 1 Tbsp Custard

8.Hiliki punje 10
 10 Cardamon pieces

9.Mafuta ya kula vijiko 3
 3 Tbsp Cooking Oil

10.Maziwa robo lita
 1/4 Litre Milk

11.Chumvi kiduchu 
 Pinch of Salt

12.Mafuta lita 1
 1 Litre Cooking

MAANDALIZI/PREPARATION

1.Chunga unga kwenye chombo unachotumia kukandia
 Sift flour through a sieve to the bowl

2.Weka chumvi,custard,siagi na mafuta vijiko viwili kwenye unga wako kisha uchanganye
 Add salt,custard,butter and 2 Tbsp of Oil into the flour then mix it well

3.Kisha weka maziwa kidogo kidogo mpaka unga wako ujishike upate donge moja
 Pour the milk little by little until you get a dough

4.Kanda unga kwa dakika 10 kisha ufunike uache kwa dakika 3
 Knead the dough till soft then cover it for 3 minutes

5.Ukande tena kwa dakika 10 nyengine kisha upake mafuta kijiko kimoja na ufunike kwa dakika 5
 Keep kneading for 10 minutes then add 1 Tbsp of Oil and cover the dough for 5 minutes

6.Kisha kata kata kwa kisu madonge makubwa kiasi kama kumi kisha yatengeneze kwa mkono yawe marefu
 Cut the dough into 10 then use your hand to make them long and thin dough(strips)

7.Weka kwenye kibao na kata kata kwa kisu vipande vya ukubwa upendao mpaka uyamalize
 Take a knife cut each strips into smaller pieces

8.Twanga hiliki zako weka pembeni
 Crush the cardamon well and keep them aside
 
JINSI YA KUPIKA
Visheti
1.Weka mafuta kwenye karai yaache yapate moto kiasi
 Add the Oil into pan and let it heated

2.Kisha weka visheti vyako tumia mwiko wa kukaangia kuviachanisha
 Add the Visheti use Spartula to make sure they are not binded

3.Vipike vikiwa vya rangi ya brown vitoe acha vichuje mafuta kwenye chujio au tissue
 Cook them until they are in brown colour and remove them into the pan to the sieve

Shira(Sugar Syrup)   
1.Weka sukari,hiliki,arki kwenye sufuria na maji
 Into another Pan add Sugar,cardamon,water and Vanilla and Ice Cream Essence

2.Acha ichemke ikianza kutoa mapovu tu mimina visheti vyako
 Let it boil when it start to forms bubbles add your Visheti

3.Vipete visheti vyako kisha virudishe kwenye moto
 Take the spartula and mix the Visheti 

4.Endelea kuvipeta na kurudisha jikoni mpaka sukari igande na iwe nyeupe kwenye visheti
 Hold the two ends of the pot and flipping the visheti in the pot away from the heat until coated with syrup and turn into white colour

5.Viache vipoe tayari kula vyenyewe au na kahawa
 Let it cool and you can serve with coffee

Angalizo:Note
1.Kama unapenda visheti Vigumu unga usikande mlaini kama unapenda vilaini basi unga ukande mlaini kidogo
 If you like non soft visheti do not knead the dough till soft

2.Hakikisha unafata kipimo cha maji ya shira maana ukiweka maji mengi basi shira haitoganda
 Make sure you follow the exactly syrup measurement beacuase too much water may result light syrup and will not coat the outside of visheti

3.Shira ya visheti haiachwi ikachemka sana ikianza kufanya mapovu tu unavimimina
 Do not over cook the syrup once bubble started pour your visheti immediately

4.Visheti vidogo haviwekwi hamira
  Do not add yeast in this type of visheti

Furahia Visheti Vyako

Maoni 2 :