MAHITAJI
1.Mchele robo
2.Nyama Robo
3.Nyanya(Tungule)
kubwa 3
4.Karoti 1
5.Pilipili boga
(Pilipili Hoho) 1
9.Kitunguu maji
kidogo 1
10.Nyanya pakti
vijiko vya chakula 3
11.Vitunguu thomu
punje kubwa 3
12.Chumvi kiasi
13.Mafuta vijiko vya
chakula 3
14.Tangawizi
iliotwangwa kijiko cha chakula 1
15.Viazi mbata
vidogo 6
16.Maji kikombe
kikubwa cha chai 1
MAANDALIZI
1.Katakata nyama
yako na ioshe
2.Chagua mchele na
uoshe vizuri
3.Osha viungo
vilobakia na viache ndani ya bakuli lenye maji
4.Anza kukata kata
vitunguu weka pembeni
5.Katakata pilipili
boga weka pembani
6.Kisha katakata karoti kwa urefu nayo iweke pembeni
7.Menya viazi
mbatata na weka pembeni
JINSI YAKUPIKA
1.Weka nyama
tangawizi na vitunguu thomu vilotwangwa na chumvi jikoni acha kwa
dakika 2
2.Weka maji kiasi
acha iive
3.Endelea kuweka
maji mpaka iive na kuwa laini na iache na supu kidogo sana
4.Weka sufuria
nyengine jikoni na weka mafuta
5.Kaanga
vitunguu,karoti na pilipili boga
6.Weka viazi viache
kwa dakika 1
7.Kisha weka nyanya
na chumvi na koroga kisha funika kwa dakika 3
8.Mimina supu yako
acha kwa dakika 5 ukiwa umefunika
9.Weka nyanya ya
paketi koroga acha kidogo
10.Mimina Maji
yaache yachemke vizuri
12.Onja chumvi kama
kidogo Ongeza kisha weka mchele wako
13.Koroga kidogo
funika mchele wako mpaka maji yakauke
14.Geuza wali wako
upambie au ufunike hadi ukauke
15.Ukikauka tayari
kwa kuliwa
16.Unaweza kula na
salad ama mtupu
Angalizo:
1.Hakikisha unaweka
mchele wakati maji yamepungua ili usiwe bwabwa
2.Usikoroge wali
mara kwa mara
3.Usiweke maji mengi
ukiwa bwabwa haupendezi
Furahia Wali
Wako.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni