MAHITAJI
1.Ndizi mbivu 2
2.Maziwa pakti 1
3.Sukari kijiko cha
chakula 1
4.Arki Vanilla
kijiko cha chai 1
5.Custard kijiko cha
chakula 1
9.Vipande vya barafu
MAANDALIZI
1.Osha ndizi zikiwa
na maganda yake vizuri
2.Menya ndizi na
uikate kisha weka kwenye jagi la blender
4.Mimina maziwa
kwenye ndizi
5.Weka
sukari,custard na arki
6.Malizia kuweka
barafu zako
JINSI YA KUTENGENEZA
1.Chukua jagi weka
kwenye blender
2.Kisha saga
mchanganyiko huo kwa dakika kadhaa
3.Rudia kusaga kwa
mara ya pili ikisagika vizuri mimina kwenye gilasi
4.Chukua mrija
tayari kwa kunywa
Angalizo:
1.Kama huna barafu
saga na maziwa ya baridi
2.Ukipenda ya baridi
sana weka kwenye friji
3.Kama mchanganyiko
mzito sana weka maji kidogo
4.Sio lazima kuweka
sukari
Furahia Kinywaji
Chako.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni