MAHITAJI
1. Tambi Nyembamba Pakti 1
2. Sukari Glasi Ndogo1
3. Hiliki Kiasi
4. Arki Vanilla Kijiko 1
5. Zabibu Kavu Kiasi
6. Mdalasini mzima kiasi
7. Mafuta Ya Kukaangia Robo
Kikombe
8. Maji Glasi Kubwa 2
MAANDALIZI
1. Pasua
tambi zako weka pembeni
2. Menya
hiliki kisha zitwange
JINSI YA KUPIKA
1.Weka mafuta kwenye sufuria anza kukaanga
tambi zako mpaka ziwe na rangi ya brown
2. Kisha weka maji,hiliki,sukari,mdalasini,zabibu
na arki vanilla
3. Koroga kidogo kuchanganya tambi zako
4. Funika acha zichemke mpaka zikauke
5. Zikikauka funika na mkungu weka mkaa juu
yake kama unavyo pika wali acha zikauke vizuri
6. Baada ya dakika 10 epua.
7. Changanya vizuri kisha pakua.
Angalizo:
1.Ili tambi ziwe nzuri hakikisha maji hayawi mengi ili ziweze kuchambuka.
2.Unaweza kuongeza sukari kama mpenzi wa sukari
Furahia Tambi Zako
Ntafanyaje zikiwa ngumu
JibuFutaNtafanyaje zikiwa ngumu
JibuFuta