Matunda ni mojawapo wa kundi la vyakula, ni muhimu sana kwa afya bora.
Matunda yakitengenezwa vizuri yanavutia sana na yanakuwa ni chakula
kizuri sana.
Mahitaji
Embe iliyoiva kiasi
Nanasi
Tango
Tikiti maji
Zabibu
Papai
Matayarisho
1. Ondoa maganda kwenye embe, nanasi, tango, papai na tikiti maji kisha kata kata vipande vidogo vidogo vya mraba
2. Changanya vipande vya matunda kwenye bakuli safikisha weka na zabibu zilizotolewa kwenye kikonyo chake.
3. Weka kwenye friji yapate ubaridi kidogo
4. Saladi yako tayari kwa kuliwa
Waweza kula saladi hii kama mlo wa kati au kama mlo kamili wa usiku.
Enjoy!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni