MAHITAJI
1.Unga wa ngano nusu kilo
2.Mtindi wa ml 750
3.Chumvi kijiko cha chakula 1na nusu
4.Sukari nusu kijiko cha chakula
5.Samli kikombe kidogo cha chai nusu
6.Mafuta ya kupikia nusu kikombe
7.Maganda ya Chungwa kijiko cha chakula 1
8.Juice ya chungwa vijiko 4
9.Maziwa ya unga robo kikombe
10.Ute wa mayai 2
11.Kungu manga(sio lazima)
MAANDALIZI
1.Chunga unga wako weka kwenye chombo cha kukandia
2.Weka chumvi,maziwa,maganda ya machungwa changanya weka pembeni
3.Chukua mtindi,weka sukari na juice ya chungwa piga piga na umma mpaka uchanganyike vizuri
4.Tia ute wa yai kwenye unga wako changanya na mwiko unga wako vizuri
5.Weka mtindi kwenye unga wako na uchanganye vizuri kisha ukande kwa dakika 5 mpaka ulainike
6.Funika unga wako kwa dakika 10 kisha uweke samli vijiko 3 endelea kuukanda mpaka uwe unavutika kwa dakika 10
7.Kisha funika tena kwenye container kwa muda wa nusu saa
8.Katakata madonge kulingana na size ya chapati unayoitaka
9.Sukuma madonge yako duara kisha yapake samli kati na sokota na uyapange kwenye bakuli lenye mfuniko na uyaache kwa nusu saa
10.Baada ya hapo utaanza kusukuma duara kwa ajili ya kupika chapati
JINSI YA KUPIKA
1.Yeyusha samli ilobaki changanya na mafuta
2.Weka kikaangio chako jikoni hakikisha moto ni wa wastani
3.Weka chapati yako mpaka ifanye brown
4.Geuza Chapati yako upande wa pili ikiwa ya brown weka mafuta kijiko kimoja
5.Izungushe chapati yako huku ukiikandamiza na kijiko ili kuilainisha kati mpaka nchani
6.Toa chapati weka nyengine mpaka umalize chapati zako
NB: 1.Ili chapati ziwe laini hakikisha unakanda kwa muda mrefu mpaka zinalainika
2.Ipe mda wa kutulia kabla kuipika
3.Usipende kuiweka mafuta mengi wakati wa kupika
4.Usigeuze geuze mara kwa mara wakati wa kuchoma
Furahia Chapati Zako.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni